
Viongozi wa mapinduzi nchini Niger, wamesema watamfungulia mashtaka ya uhaini na kuzorotesha usalama nchini humo, Rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum, ambapo wamebainisha kuwa tayari wamekusanya ushahidi utakaotumika kumshitaki Rais huyo na washirika wake, kwenye vyombo vinavyoaminika kitaifa na kimataifa.
.
Akisoma taarifa hiyo, Kanali Meja Amadou Abdramane kupitia televisheni ya taifa, amesema kuwa Bazoum bado anaweza kuwasiliana na watu wa nje kwa kuwa hawajazuia mawasiliano kwenye kasri hilo la Rais, pia anakutana na daktari wake kila wakati kwani hata Jumamosi hii alikutana nae na taarifa ya daktari huyo ilisema familia yote haikuwa na tatizo lolote la kiafya.
