
Waziri wa TAMISEMI, Mhe.Angelah Kairuki amesema Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan, ameagiza nyumba ya mwalimu mlezi wa wanafunzi (Patron) katika shule ya Sekondari Azania ijengwe mara moja ili mwalimu huyo awepo wakati wote kusimamia wanafunzi wanaokaa bweni katika shule hiyo.
.
Waziri Kairuki ameyasema hayo wakati akikabidhi magari 10 ya Maafisa Elimu Sekondari, yaliyonunuliwa kupitia mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R), ambapo amebainisha kuwa watatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo na changamoto zingine watazitatua kwa kadri fedha inavyopatikana.
