Back to top

PRIGOZHIN AHOFIWA KUFARIKI KWENYE AJALI YA NDEGE

23 August 2023
Share

Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Urusi imesema Bosi wa Jeshi la Wagner, Yevgeny Prigozhin, anahofiwa kufariki dunia, baada ya jina lake kuonekana kwenye orodha ya abiria wa ndege iliyoanguka na kusababisha vifo vya abiria wote waliokuwa kwenye ndege hiyo.
.
Kupitia channel ya Telegram inayounganishwa na Jeshi la Wagner, Gray Zone imeripoti kuwa ndege aina ya Embraer ilidunguliwa na walinzi wa anga katika mkoa wa Tver, kaskazini mwa Moscow.
.
Ndege hiyo iliyokuwa ikiruka kutoka Moscow kwenda St Petersburg, ilikuwa imebeba abiria saba na wafanyakazi watatu.
.
Prigozhin aliongoza jaribio la uasi ambalo alilisitisha muda mfupi baadae dhidi ya vikosi vya Jeshi la Urusi mnamo Juni, mwaka huu, hatua ambayo Rais Wa Urusi Vladmir Putin alisema ni uhaini na kuahidi kuwaadhibu wote waliohusika. #via #BBC