
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar, Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi kwa kuendelea kuipa kipaumbele Sekta ya Afya.
.
Mhe.Othman Masoud Othman, ameyasema hayo wakati akizindua Mpango wa Uwekezaji katika Afya ya Mama na Mtoto Tanzania wa miaka mitano (Tanzania Martenal & Child Health Investment Program) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia pamoja na Shirika la Global Financing Facility wenye lengo la kuimarisha afya ya Mama na mtoto nchini.
.
Mpango huo ambao uwekezaji wake utagharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 275, ambapo kiasi cha dola za Marekani milioni 250 ni mkopo wa gharama nafuu kutoka Benki ya Dunia na kiasi cha dola za Marekani milioni 25, kutoka Global financing facility, utatekelezwa chini ya Usimamizi wa Wizara ya Afya Tanzania Bara, Wizara ya Afya Zanzibar pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI.
