Back to top

MIGAHAWA YA 'SUPU YA MBWA' YAPATA HOFU INDONESIA

24 August 2023
Share

Kufuatia baadhi ya mamlaka za mitaa, kupiga marufuku biashara ya nyama ya mbwa, ikiwemo mishikaki na supu ya mnyama huyo, wamiliki wa migahawa inayofanya biashara hiyo wameingiwa na hofu, baada ya mauzo kuanza kushuka.

Mwezi uliopita, Mamlaka ya Sulawesi Kaskazini nchini humo, ilitangaza kupiga marufuku kuchinja na uuzaji wa nyama ya mbwa na paka uliokithiri katika Soko la Tomohon,  ambalo kwa muda mrefu limekuwa na sifa mbaya kama kivutio cha kitalii na ishara ya ukatili wa wanyama.

Caroll Senduk, Meya wa jiji la Tomohon, alitangaza marufuku ya biashara hiyo, baada ya miaka mingi ya kampeni ya watetezi wa ustawi wa wanyama ambao walidai kuwa biashara hiyo ilikuwa ya kikatili na hatari ya kueneza kichaa cha mbwa.