
Rais wa Urusi, Vladimir Putin amevunja ukimya wake kuhusu kifo kilichoripotiwa cha Yevgeny Prigozhin ,baada ya ndege ya kibinafsi ya chifu Wagner kuanguka.
Amesema mkuu wa kundi la Wagner alikuwa "mtu mwenye talanta" ambaye "alifanya makosa makubwa maishani".

Bw Putin pia alituma salamu za rambirambi kwa familia za watu wote 10 wanaosemekana kuwa ndani ya ndege hiyo iliyoanguka kaskazini-magharibi mwa Moscow Jumatano jioni.
Hata hivyo Wizara ya Ulinzi ya Uingereza, inasema ingawa hakuna uthibitisho wa uhakika kuwa Kiongozi wa Wagner, Yevgeny Prigozhin , alikuwa ndani ya ndege iliyoanguka, kuna uwezekano mkubwa amekufa.
