
Serikali imezitaka Taasisi zinazosimamia bidhaa za afya ikiwemo Dawa, vifaa tiba pamoja na vitendanishi kuwasaidia Wafanyabiashara wa bidhaa hizo kufanya biashara kwa mujibu wa Sheria na taratibu badala ya kuwa vikwazo ili wananchi wanufaike na bidhaa hizo kwa gharama nafuu na kwa ubora unaotakiwa.
.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel, wakati akifungua mkutano wa wawekezaji wa bidhaa za dawa na Wafamasia, wenye lengo la kuwakutanisha Wafanyabiashara hao ili kujadili changamoto na mbinu mbalimbali za kuboresha upatikanaji wa bidhaa hizo na kwa gharama nafuu.
.
Mhe.Mollel amebainisha kuwa itaendelea kuboresha mazingira kwa wawekezaji kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi ili Watanzania wenye hali zote wanufaike na huduma za dawa na vifaa tiba kwa ubora na gharama nafuu.
