
Rais wa Shirikisho la soka nchini Uhispania, Luis Rubiales amesimamishwa na FIFA kwa kipindi cha siku 90 cha awali.
Rubiales alimbusu kiungo Jenni Hermoso kwenye mdomo, wakati wa sherehe ya medali ,baada ya Uhispania kushinda fainali ya Kombe la Dunia la Wanawake,na kudai kuwa ,busu hilo lilikuwa la makubaliano lakini Hermoso anasema haikuwa hivyo.
Fifa inasema, mbali na kupewa adhabu ya kusimamishwa kushiriki kwa shughuli zote za mpira wa miguu, sio Rubiales wala Shirikisho la kandanda wanaruhusiwa kuwasiliana na Hermoso.
Shirikisho la soka la Uhispania hapo awali lilisema litachukua hatua za kisheria kutokana na maoni aliyotoa Hermoso.
Takriban wachezaji 81 wa kike walisema hawataichezea timu ya taifa kama Rubiales akiwa bado yuko kazini.Luis Rubiales amekataa kujiuzulu na kutoa maneno likiwemo la "atapigana hadi mwisho".
