Back to top

WAZUIENI WASIFUNGE BIASHARA ZA WATU -DKT.NCHEMBA

28 August 2023
Share

Waziri wa Fedha, Mhe.Mwigulu Nchemba, amewataka Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa, wasimamie ipasavyo shughuli za biashara katika maeneo yao.

Amewataka wawazuie watendaji wa taasisi za serikali kufunga biashara za watu, kunapojitokeza mizozo ya ukusanyaji kodi, tozo na mambo mengine kwa sababu kitendo hicho kina athari kubwa kiuchumi na ajira za watu.

Amerejea rai yake kwa watendaji wa serikali ya kuacha kufunga biashara za watu kunapotokea ukiukwaji wowote wa sheria za ukusanyaji wa kodi, ada na tozo kwa sababu kitendo hicho kinaathiri uchumi wanchi na ajira za wananchi, mapato ya kampuni na mapato ya serikali.

Waziri Mwigulu ametoa maagizo hayo katika mada kuhusu Hali ya Uchumi wa Nchi na Utekelezaji wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024, kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa wa mikoa yote kwenye semina iliyofanyika Katika Shule ya Uongozi ya Julius Nyerere, Kibaha mkoani Pwani.


Aiodha, amewahimiza waweke usimamizi madhubuti wa ukusanyaji wa mapato na matumizi ya fedha za umma katika maeneo wanayoyasimamia, ili kufikia malengo na kuwezesha juhudi za serikali katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati na ujenzi wa miundombinu wezeshi kwa ajili ya utoaji wa huduma za msingi za kijamii ikiwemo elimu, afya na maji safi na salama.

Amesema katika mwaka wa Fedha wa 2023/24, serikali inatarajia kukusanya shilingi trilioni arobaini na nne nukta tatu tisa kutoka vyanzo vyake vyote.