
Kijana aliyejitambulisha kwa jina la Mussa Mawa, amekamatwa katika maeneo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili akijihusisha kutapeli wananchi wanaopata huduma kwa kujifanya daktari, ambapo Mkuu wa Idara ya Ulinzi kwenye Hospitali hiyo, Bw. Alfred Mwaluko, akabainisha kuwa walimbaini daktari huyo feki akiwa kwenye harakati za kuwatapeli wananchi wanaouguza ndugu yao aliyelazwa jengo la Mwaisela.
.
Kufuatia tukio hilo Hospitali hiyo imetoa rai kwa wote wanaojihusisha na kutapeli wananchi katika eneo hilo, kwani kwa sasa ulinzi umeimarishwa na wakijaribu kufanya hivyo watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya usalama.
