
Zaidi ya watu 70, wameripotiwa kufariki dunia, huku wengine wakijeruhiwa baada ya jengo la ghorofa 5, lililopo katikati mwa Jiji la Johannesburg, nchini Afrika Kusini, kuungua moto, huku ripoti zikionyesha kuwa, watu wengi waliokuwa ndani ya jengo hilo ni wahamiaji kutoka mataifa mengine ya Afrika.
.
Wakizungumza na #BBC Maafisa wa Jiji hilo, wamesema chanzo cha moto huo bado hakijajulikana, lakini wameweza kuwatoa baadhi ya watu waliokuwa ndani na kwamba wanaendelea kuwatafuta waathiriwa wengine. #via #BBC
