Back to top

WAPIGWA RISASI WAKIJARIBU KUVAMIA KITUO CHA MAFUTA

03 September 2023
Share

Jeshi la Polisi Mkoa Njombe limefanikiwa kuwakamata majambazi watatu, baada ya kuwajeruhi kwa kuwapiga risasi, walipokuwa wakijaribu kuvamia kituo cha mafuta cha ORYX, kilichopo Mtaa wa Mjimwema, Mjini Njombe, jirani na kituo kikuu Cha mabasi Cha Mkoa wa Njombe.

.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo John Imori, amesema waliamua kuwapiga risasi majambazi hao, baada yakukataa kutii amri halali ya Jeshi hilo, iliyowataka walale chini.