Back to top

URUSI YASHAMBULIA BANDARI YA NAFAKA UKRAINE

04 September 2023
Share

Urusi imefanya shambulio kwa kutumia ndege nyuki (drones) kwenye moja ya bandari kubwa za kuuza nafaka za Ukraine, masaa kadhaa kabla ya mazungumzo ya Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan.

Jeshi la anga la Ukraine, mapema Jumatatu liliwataka wakazi wa bandari ya Izmail, moja wapo ya vituo vikuu vya kuuza nafaka nchini kwenye Mto Danube katika mkoa wa Odesa, kutafuta makazi.

Gavana wa Odesa Oleh Kiper baadaye alisema ndege nyuki (drones) 17 ziliagushwa katika mkoa wa Kusini, lakini  shambulio hilo lilisababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ya bandari.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, amepanga kukutana na Vladimir Putin leo, akitumaini kumshawishi kiongozi huyo wa Urusi ajiunge tena na mpango wa nafaka wa Bahari Nyeusi.