Back to top

MAFUTA YASABABISHA KIFO CHA BODABODA, MARA

05 September 2023
Share

Moris Ally, mwenye umri wa miaka 30, Mkazi wa Mtaa wa Bukanga, uliopo Manispaa ya Musoma, mkoani Mara, ambaye ni mwendesha bodaboda, amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na mlinzi wa kituo cha mafuta cha White Company Limited, Bw.Yusuph Gamba, baada ya ugomvi kati yake na kijana huyo. 
.
Akizungumza juu ya tukio hilo Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara Disimas Kisusi, ameeleza kuwa Kijana huyo alifika kwenye kituo hicho na kuhudumiwa mafuta lakini alianza kuongea na ndugu yake waliyekutana naye kwenye kituo hicho, ndipo mtoa huduma alipomtaka kusogea mbali lakini alikaidi hali iliyopelekea ugomvi ambao uliamliwa na mlinzi, ambaye naye baadae walianza kupigana hadi mlinzi kuchaniwa sare zake na kuamua kwenda kuchukua bunduki kwa mlinzi mwenzie kisha kumpiga risasi ya mgongoni kijana huyo.