
Shabiki wa Manchester United mjini Eldoret, nchini Kenya, amekimbizwa hospitalini baada ya kujaribu kula trei la mayai ya kuchemsha, baada ya kuwekeana dau (ku-bet) na marafiki zake wa Arsenal.
Thomas Kiptanui Kemboi, almaarufu Kapkeno, waliwekeana dau na marafiki zake ambao ni mashabiki wa Arsenal wikiendi wakati timu hizo mbili zilipocheza.
Kapkeno aliweka dau la kula trei nzima ya mayai ya kuchemsha iwapo Man United wangeshindwa na Arsenal, na waliposhindwa ilibidi atimize ahadi.
Hata hivyo, alipofika yai la 15, Kapkeno alianguka, huku marafiki wakicheka, lakini mambo yaligeuka haraka walipogundua kuwa alikuwa amezidiwa.
Walimkimbiza hospitalini ambako aligundulika kuwa na tatizo la kuvimbiwa alitibiwa na kuruhusiwa.
