Back to top

RAIS MWINYI AKOSHWA NA PROGRAMU YA BBT

07 September 2023
Share

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi, ameonesha kufurahishwa na Programu ya Jenga Kesho Iliyobora (BBT), ambapo amebainisha kuwa programu hiyo ni moja ya suluhu ya kutatua changamoto nchini.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo wakati akiongea na wadau kwenye mkutano wa kuonesha fursa za uwekezaji kwenye programu ya kielelezo ya Jenga Kesho Iliyobora (BBT) ambao umefanyika Dar es Salaam Septemba 7, 2023. 

Aidha Mhe. Dkt. Mwinyi ameongeza kuwa mkutano huo umelenga kuonesha fursa kwa wadau na kuwahamasisha kuunga mkono programu hiyo ya BBT.

Mkutano huo ni sehemu ya Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika (AGRF) unaoendelea jijini Dar es Salaam.