Back to top

WANANCHI WAPIME AFYA ZAO KUBAINI UGONJWA WA SELIMUNDU

11 September 2023
Share

Wananchi katika mikoa ya Kanda ya Magharini na Kanda ya Ziwa, wametakiwa kupima afya zao, ili kubaini kama kuna viashiria vya ugonjwa wa Selimundu, kwa lengo la kuwaondolea adha watoto watakaozaliwa katika ndoa.

Daktari bingwa wa watoto katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Dkt.Amon Ryakitimbo ametoa rai hiyo alipozungumza na waandishi wa habari mjini Tabora juu ya athari za ugonjwa huo ili waweze kutumia vyombo vyao kuielimisha jamii.

Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa hospitali hiyo, Kaimu Mkurugenzi Dkt.Renatus Burashahu, amesema mkoa wa Tabora ambao ni moja ya mikoa inayokabiliwa na tatizo hilo, umeanza kampeini ya kuwaelimisha wananchi kuhusu ugonjwa huo ili wajue namna ya kuuzuia.