Back to top

MRADI WA SAMIA UPELEKWE MAJIJI MAKUBWA YENYE UHITAJI

11 September 2023
Share

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa, amelipongeza Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa utekelezaji mzuri wa miradi yake katika maeneo mbalimbali, lakini shirika hilo linatakiwa kupeleka mradi wa Samia wenye sura ya kitaifa kwenye majiji makubwa yenye uhitaji wa nyumba.

Waziri Silaa ameeleza hayo Jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza mara baada ya kukagua miradi ya 711 Kawe, Samia Housing Scheme Phase I pamoja na mradi wa Morocco Square.

"Nataka mradi wa Samia uende kwenye mikoa mingine yenye uhitaji na kuwa na mradi wenye jina la Samia lazima uwe na sura ya kitaifa kuwe na kuwe na plan kubwa ya maeneo mengi"Amesema Silaa.

Waziri Silaa ameeleza kuridhishwa na maendeleo ya mradi wa mradi wa Morocco Square, ameeleza kuwa, umefikia wakati sasa kwa shirika la NHC kuongeza uwekezaji wa miradi ya nyumba ili watanzania wapate nyumba za kupanga na kununua.

"Tuna nyumba nyingi katika prime area ni nyumba za chini anakaa mpangaji mmoja  ni wakati sasa kuongeza uwekezaji katika miradi ya nyumba ili ifike wakati nyunba ziwe nyingi na watanzania wengi wapate nyumba za kununua na kupanga"Amesema Waziri Silaa.

"Ninyi mnafahamu pressure ya nyumba za NHC ni kubwa na hizi re-development mhakikishe mnatengeneza mpango wa kuwa maeneo yote, tunataka kuona Upanga, City Centre ikiwa na nyumba, wale waliokiwa wanajenga miaka ile ya 70 na 60 zile nyumba za ghorofa 3 walikuwa wanajenga kwa popukation ya watu milioni 3 na sasa tuko milioni 61 tunatarajia re-development inafanyika kwenye maeneo mengi yenye uhitaji"Amesema.

Akigeukia mradi wa 711 Kawe uliosimama kwa muda mrefu, Waziri Silaa amesema angependa kuona ndoto ya Rais Samia inatimia kwa kukamilika mradi huo.

"Kusimama kwa mradi ni changamoto na kikubwa ni kuhakikisha mazungunzo yanafika mwisho kwa kuwa kuendelea kuchelewa gharama inaongezeka. Nitahakikisha mazungumzo yanafika mwisho na mradi unaendelea Oktoba 2023, mradi uishe na ulete faida na tija kwa uchumi" Amesema.

Aidha, Silaa amegusia sera ya ubia ya NHC ambapo alisema shirika hilo linatakiwa kuangalia mpango huo na kueleza kuwa, haiwezekani kuendelea wenyewe ndani ya taifa kwa kutegemea mitaji ya ndani au mikopo ya benki.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Hamad Abdalah ameeleza kuwa mradi wa Moroko square umeenda vizuri kutokana na maeneo ya jengo hilo kupangishwa ambapo alisema kati ya nyumba mia moja za mradi huo nyumba arobaini tayari zimepangishwa.