Back to top

SONGWE: WATOTO ZAIDI LAKI 4 KUPATA CHANJO YA POLIO

12 September 2023
Share

Wizara ya Afya imesema watoto zaidi ya 400,000, wenye umri chini ya miaka 8, wanatarajia kupata chanjo dhidi ya ugonjwa wa Polio, mkoani Songwe, ambapo imebainisha kuwa, imefikia hatua hiyo baada ya mtoto mmoja kukutwa na ugonjwa huo, ambao mnamo mwaka 2015, Tanzania, ilitangazwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), kuutokomeza.
.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya,  Mhe. Ummy Mwalimu, akiwa katika ziara ya kukagua utoaji wa huduma za Afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Songwe.

.

“Baada ya kupatikana kwa mtoto Mmoja mwenye ugonjwa wa Polio tumeamua kutoa chanjo ya ugonjwa huo ambapo kwa Mkoa wa Songwe tunatarajia kuchanja watoto takribani Laki Nne ambao wana umri chini ya Miaka Nane”. Amesema Waziri Ummy 

Aidha, Waziri Ummy amesema kutokana na hatari iliyopo, Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais TAMISEMI imeamua kuendesha kampeni maalumu ya kutoa chanjo ya kuwakinga watoto dhidi ya ugonjwa wa Polio.