
Zaidi ya watu 5,300 hadi sasa wamethibitishwa kufariki na wengine takriban 30,000 wakilazimika kuyahama makazi yao kufuatia mafuriko yaliyolikumba eneo la mashariki mwa Libya siku ya Jumapili, baada ya mabwawa mawili kupasuka, huku kukiwa na hofu kuwa huenda watu 20,000 wamefariki katika mafuriko hayo, kutokana na idadi ya wilaya zilizoathiriwa.
.
Kufuatia maafa hayo, imeripotiwa kuwa Serikali mbili zinazohasimiana nchini humo zimeungana kuratibu juhudi za kutoa msaada kwa waathirika wa mafuriko. #via #bbc
