
Mwanafunzi wa darasa la nne, mwenye umri wa miaka 12 katika Shule ya Msingi ya Sare huko Awendo, Kaunti ya Migori nchini Kenya, amejiua ndani ya darasa lake Jumanne, Septemba 19 asubuhi.
Jeshi la Polisi, wameanzisha uchunguzi kufuatia kifo cha mwanafunzi huyo, ambaye mwili wake ulikutwa ukining'inia, ndani ya darasa na wanafunzi waliokuwa wameripoti shuleni ambapo chanzo cha kifo hakijajulikanampaka sasa hawajajua.
Mama wa mtoto huyo, alisema mwanafunzi huyo aliondoka nyumbani asubuhi , na hakueleza tatizo lolote alilokuwa nalo.
Wakati huo huo chifu wa eneo hilo Paul Ogweno, ametoa wito kwa wazazi kuwa na mazungumzo ya mara kwa mara na watoto wao, ili waweze kujua baadhi ya changamoto wanazopitia.
