Back to top

WAZAZI WALINDENI WATOTO, DUNIA IMEHARIBIKA

20 September 2023
Share

Wazazi na walezi wametakiwa kuhakikisha wanawalinda watoto dhidi ya vitendo vya kikatili kwa kuhakikisha wanatoa taarifa ili hatua za kisheria zichukuliwe badala ya kuwa sehemu ya kuwaficha watu wanaofanya vitendo hivyo vinavyosababisha madhara makubwa kwa watoto. 
.
Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama, wakati akizungumza na wakazi wa Kata ya Kilagano, iliyopo wilayani Songea Vijijini, mkoani Ruvuma.
.
Mhe. Mhagama amesema vitendo vya ukatili vimekuwa vikikithiri kila kukicha maeneo mbalimbali huku baadhi ya vitendo hvyo vikifanywa na  wazazi wenyewe, walezi na hata watu wa karibu ambao wanategemewa na jamii kuwa sehemu ya kuwajenga watoto katika malezi bora.
.
“Dunia imeharibika na wala siyo siri na lazima tuelezane walindeni hao watoto tutadaiwa na Mwenyezi Mungu, lazima tuwe waangalifu jengeni tabia ya kuwafuatilia watoto kila wanapotoka shule  mtoto anafananaje, anaonesha na tatizo? msikilize na kina mama wenzangu mjenge urafiki na watoto siyo mtoto anakusogelea unakuwa  mkali hutaki kumsikiliza,”Amesisitiza Mhe. Jenista.