Back to top

WATOTO 90, WALISHWA KEKI ZENYE BANGI

22 September 2023
Share

Watoto 90 wa shule moja ya msingi nchini Afrika Kusini wamepelekwa hospitalini baada ya kula keki zinazodhaniwa kuwa zimechanganywa na bangi.

Maafisa wamesema wanafunzi hao walinunua keki hizo kutoka kwa wachuuzi wa barabarani walipokuwa wakielekea Shule ya Msingi ya Pulamadibogo, Kaskazini-Magharibi mwa Pretoria.

Watoto hao walipata kichefuchefu, maumivu ya tumbo na kutapika ambapo wasichana watatu bado wako hospitalini.

Watu wawili wamekamatwa na wanakabiliwa na mashtaka ya kujaribu kuua.

Washukiwa hao wenye umri wa miaka 21 na 19, watafikishwa Mahakamani, polisi wamethibitisha.