Back to top

DKT.NDUMBARO AJIUZULU KAMATI YA RUFAA YA TFF

22 September 2023
Share

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dk. Damas Ndumbaro amejiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa Kamati ya Rufani ya Leseni za Klabu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF).
.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Shirikisho hilo imebainisha kuwa Mhe.Ndumbaro, aliamuandikia barua Rais wa TFF, iliyoeleza kuwa, imemlazimu kujiuzulu kwenye nafasi hiyo, ili aweze kutekeleza majukumu yake mapya kama Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa haki na kuepeusha mgongano wa maslahi.