Back to top

RUFAA ZA MATIBABU YA NJE YA NCHI ZAPUNGUA KWA ASILIMIA 97

23 September 2023
Share

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwini Mollel, amesema Rais Dkt. Samia ametoa kiasi cha shilingi Tirioni 6.7 ili kuboresha Huduma za afya nchini, kwa kuwezesha upatikanaji wa vifaa tiba, dawa na vitendanishi, uboreshaji wa miundombinu, kuongeza wataalamu wa afya na kusomesha waataalam kupitia programu ya Samia Scholarship.

Naibu Waziri Dkt. Mollel ameyasema hayo, wakati alipo mwakilisha Waziri Mkuu katika uzinduzi wa kiwanda cha kutengeneza vitendanishi Action Medeor Kibaha Mkoani Pwani nakuongeza kuwa mapinduzi ya Mh.Rais katika sekta ya afya yamepunguza Rufaa za nje ya nchi kwa asilimia 97.


Naibu Waziri Amesema kuwa majengo ya Huduma za dharura 128 na majengo ya wagonjwa maututi 78 yamejengwa kwa mwaka 2023, hivyo ni jukumu la wataalamu wa afya kuhakikisha wanavitunza vifaa tiba vizuri ili kuwahudumia wananchi katika ubora unao stahili ambapo pia amesema kwa sasa kanda zote zina Mashine ya MRI mbili kwa ajili ya kutoa Huduma katika kanda hizo na mashine moja ni Bilioni 3.

Aidha Dkt. Mollel amewataka TMDA na MSD kuhakikisha wanafika katika kiwanda hicho na kutatua changamoto zilizopo ili kuwezesha kiwanda hicho kufanya uzalishaji kwa ufasaha.

Akizungumza kwa Niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majali , Dkt. Mollel amesema Waziri Mkuu ametoa shilingi milioni 4 kwa vijana sita wabunifu kutoka chuo cha DIT ili kuwatia moyo kuendelea kuwaza mambo makubwa ya kulisaidia taifa hili katika kupiga hatua ya kiteknolojia na maendeleo kwa ujumla.