
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Wilbrod Mutafungwa amewaonya watu wanaofanya uhalifu ndani ya Ziwa Victoria, ikiwemo Uvuvi haramu huku akiahidi kwamba Jeshi la Polisi halitomvumilia mhalifu.
Kamanda Mutafungwa ametoa kauli hiyo wakati akitoa elimu ya kuzuia uhalifu kwa wananchi wa Kata ya Bugogwa, Sangabuye, Shibula na Kayenze Wilayani Ilemela mkoani humo.
Kamanda Mutafungwa ametangaza wakati mgumu kwa wahalifu wanaopora vyavu za wenzao na mazao ya uvuvi huku akiahidi hatua kali za kisheria kuchukuliwa dhidi ya wahusika.
Ameomba ushiriki wa jamii kutokomeza vitendo hivyo kwa kile alichosema usalama wa nchi unalindwa na kila mwananchi ili kuwezesha shughuli za maendeleo kuendelea nchini.
