Back to top

Wawili mbaroni kwa kuratibu maandamano mtandaoni April 26.

21 March 2018
Share

Jeshi la polisi mkoani Dodoma limewakamata watu wawili kwa tuhuma za kuhamasisha maandamano haramu kwenye mitandao ya kijamii, maandamano hayo haramu ambayo yamepangwa kufanyika tarehe 26 Mwezi ujao nchi nzima.

Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Polisi Gilles Muroto amewataja waliokamatwa kuwa ni AMANI CHARI, ambaye ni mfanyakazi wa mfuko wa Taifa wa bima ya AFYA - NHIF na YUDA MBATA ambaye ni mkazi wa wilayani Bahi na kuwa watafikishwa mahakamani kuanzia hivi sasa.

Kamanda MUROTO amewatahadharisha wakazi wa mkoa wa Dodoma kutojihusisha kwa namna yeyote ile na maandamano hayo haramu na atakayejihusiha nayo atachukuliwa hatua kali za kisheria.