Back to top

BOT YAWATAKA WALIOFICHA DOLA KUZIACHIA

25 September 2023
Share

Benki Kuu ya Tanzania imewataka watu walioficha dola kwa lengo la kusubiri zipande bei, ili wapate faidi kubwa waziachie zirudi kwenye mzunguko wa biashara, ili kuondoa tatizo la uhaba wa dola nchini.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bw.Emmanuel Tutuba, amesema hayo mjini Geita katika maonesho ya sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini.

Benki Kuu ya Tanzania imeshanunua zaidi ya kilo mia nne za dhahabu, kutoka kwa wachimbaji nchini, ili nchi iweze kuwa na hifadhi ya kutosha ya dhahabu.

Kwa upande wao, wataalam wa udhibiti wa kemikali zinazohatarisha afya za wachimbaji na mazingira na wataalamu wa teknolojia mpya za uchimbaji madini, wamewataka wachimbaji wadogo watumie kemikali salama, ili kulinda maisha yao.