Back to top

PAKISTANI:MPAKA NOVEMBA 1 WAWE WAMEONDOKA

04 October 2023
Share

Pakistani imewaamuru wahamiaji wote wasio na vibali, hususani raia milioni 1.73 wa Afghanistan, kuondoka kwa hiari nchini humo la sivyo watafukuzwa.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Pakistani Sarfraz Bugti amesema wamewapa mpaka Novemba 1 mwaka 2023 wawe wameondoka.

Bugti alisema takriban raia milioni 1.73 wa Afghanistan nchini Pakistan hawana hati za kisheria za kukaa huku akiongeza kuwa jumla ya wakimbizi milioni 4.4 wa Afghanistan wanaishi Pakistan.

Kuongezeka kwa mashambulizi ya wanamgambo, kwenye mpaka wa nchi hizo mbili mwaka huu kumeongeza hali ya wasiwasi.

Pakistan imelaumu mashambulizi ya watu wanaovuka mpaka, dhidi ya wahudumu wa Afghanistan mashtaka yaliyokanushwa na utawala wa Taliban.