Back to top

JELA MIAKA 25 KWA WIZI WA WATOTO KENYA

05 October 2023
Share

Fred Leparan aliyekuwa mfanyakazi katika hospitali ya Mama Lucy Kibaki ya Nairobi, Kenya amehukuhiwa kifungo cha miaka 25 jela baada ya kubainika kuuza watoto kwenye masoko kisiri.

Bw.Fred alikamatwa mwaka wa 2020 na kupatikana na hatia mwezi uliopita kwa ulanguzi wa watoto, kutelekeza watoto na kula njama ya kutenda uhalifu.

Mahakama nchini Kenya imesema Fred atatumikia kifungo cha miaka 25 gerezani, kisha atatumia miaka 10 ya kipindi cha kuchunguzwa mienendo yake.