
Takriban watu 77 wamethibitishwa kufariki katika mafuriko yaliyokumba Kaskazini Mashariki mwa India.
Mamlaka nchini humo zimesema barabara na madaraja yameharibiwa.
Mafuriko hayo makubwa yalikumba jimbo la Sikkim baada ya ziwa la barafu kupasuka ghafla.
Wanasayansi wameonya kwamba majanga kama hayo yataendelea kuwa hatari inayoongezeka katika Milima ya Himalaya kadiri halijoto ya kimataifa inavyoongezeka na barafu kuyeyuka.
Katika jimbo jirani la Bengal Magharibi, polisi wa wilaya ya Jalpaiguri wameliambia AFP kwamba mili mingine 48 imepatikana.
Zaidi ya watu 100 bado hawajulikani walipo, kulingana na takwimu rasmi.
Afisa wa idara ya kudhibiti majanga ya jimbo la Sikkim aliiambia AFP kwamba zaidi ya watu 2,500 waliokuwa wamekwama kutokana na mafuriko hayo wameokolewa.
