
Uongozi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road umetakiwa kukamilisha kwa wakati mradi wa ujenzi wa jengo la PET-CT Scan na Cyclotron (mashine ya kutengeneza mionzi ya tiba) unaogharimu kiasi cha Tsh. Bil. 18.2, ili kuleta tija ya uwekezaji uliofanywa na Serikali.
.
Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel, alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma na kuongea na menejimenti ya watumishi wa Taasisi hiyo.
.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya hiyo, Dkt. Julius Mwaiselage, amemhakikishia Dkt. Mollel kuwa mradi huo utakamilika mapema, huku akibainisha kuwa kukamilika kwake kutasaidia kutengeneza mionzi tiba ambayo huagizwa kutoka nchini Afrika Kusini, na itatumika na Taasisi hiyo na nyingine itapelekwa katika hospitali zingine hapa nchini.
