Back to top

MVUA YAUA WATU 27 NCHINI CAMEROON

10 October 2023
Share

Maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa yameua watu 27 na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa katika mji mkuu wa Cameroon Yaounde.

Wafanyakazi wa zima moto wamesema baada ya kutokea kwa maporomoko hayo, wameendelea kuwatafuta waathirika zaidi, kwani maporomoko ya ardhi  ya mara kwa mara nchini humo yamekuwa yakitokeza zaidi msimu wa mvua mjini Yaounde, ambako nyumba wakati mwingine hujengwa kwenye maeneo yasiyo sahihi katika milima ya Jiji.

Tukio hilo limetokea  katika wilaya ya Mbankolo, Kaskazini Magharibi mwa Mji wa Yaounde ambao una makazi ya watu zaidi ya  milioni tatu.

Maporomoko hayo ya Mvua kubwa iliyonyesha nchini humo yalisababisha bwawa lililokuwa limeshikilia ziwa bandia lililokuwa juu ya ardhi kupasuka, kulingana na kituo cha televisheni cha umma CRTV.