Back to top

WALIOPORA SILAHA NA KUJERUHI ASKARI WAKAMATWE

10 October 2023
Share

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Kamishna Benedict Wakulyamba, ameliagiza Jeshi la Uhifadhi (JU), kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya ulinzi na Usalama, kuhakikisha wote waliohusika na tukio la kupora silaha na kujeruhi askari wa jeshi hilo, walipokuwa wakitekeleza majukumu yao, katika Msitu wa Hifadhi Irangi wakamatwe Mara moja.

Kamishna Wakulyamba amelaani tukio hilo la kinyama lililofanywa na wananchi hao wachache wa Kijiji cha  Mafai, Wilayani Kondoa, na kusema Wizara hiyo haitavumilia uovu huo, na kuwa wote waliohusika ni lazima wakamatwe.

Kamishna Wakulyamba ametoa agizo hilo alipowatembelea askari waliojeruhiwa kwa kushambuliwa na Wanavijiji zaidi ya mia moja, wa Kijiji cha Mafai, kufanya kikao na Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Kondoa, ili kupata uelewa wa pamoja wa kukomesha huo uhalifu na mashirikiano zaidi katika uhifadhi wa Maliasili.

Kamishna Wakulyamba ameushukuru uongozi wa Wilaya hiyo kwa hatua za haraka ulizozichukuwa kupitia vyombo vya ulinzi na usalama kushirikiana na Jeshi la Uhifadhi na katika changamoto iliyotokea na  kuhakikisha  silaa iliyoporwa inapatikana na pia kwa uongozi wa Hospitali ya Kondoa mjini kuwahudumia vyema askari waliojeruhiwa.