Back to top

ISRAEL YASHAMBULIA UKANDA WA GAZA

11 October 2023
Share


Majeshi ya Israel yameendelea kufanya mashambulizi makali dhidi ya ukanda wa Gaza kwa siku ya nne mfululizo, ikilenga maeneo muhimu ya bandari na kivuko cha Rafa kinachounganisha Gaza na Misri, huku mashirika ya kiutu yakitafuta njia za kuwasaidia raia waliokwama katika vita hivyo.

Hadi sasa Idadi ya waliouawa nchini Israel imefika watu 1200, wakati zaidi ya watu 900 wameuawa kwa upande wa Gaza.

Wakati huo huo Kundi la Hamas limerusha makombora katika mji wa Ashkelon Kusini mwa Israel Kusini karibu na Ukanda wa Gaza, ambao ni eneo la Wapalestina.

Shambulizi hilo limekuja saa kadhaa baada ya Hamas kutishia kushambulia mji wa Ashkelon nchini Israel, kujibu mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza na kuwataka wakazi  wa mji huo kuondoka.

Jeshi la Israel limewaonya wakazi wake wa mji wa Kusini mwa Gaza wa Ashkeloni kujihifadhi katika maeneo salama yaliyotengwa baada mashambulizi ya Hamas katika mji huo.

Zaidi ya makombora 4,500 tayari yamesharushwa kutoka Gaza hadi Israel tangu Jumamosi.