
Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), umewataka Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimali watu kushirikiana na taasisi hiyo, katika kuimarisha mifumo ya usimamizi wa masuala ya usalama na afya, katika maeneo yao ya kazi, ili kuleta tija kwa taifa.
OSHA imetoa wito huo kupitia kwa Afisa Mafunzo wake, Bw. Simon Lwaho mara baada ya kuwasilisha mada ya masuala ya usalama na afya mahali pa kazi ulioenda sambamba na zoezi la upimaji wa magonjwa yatokanayo na kazi katika Kikao kazi kinachofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha (AICC).
Aidha Mkaguzi wa Afya wa OSHA, Bi Amina Nangu amesema kuwa Wakuu hawa wa Idara za Utawala ndio watoa maamuzi katika maeneo yao ya kazi hivyo wakielewa vyema Sheria na miongozo ya usalama na afya mahali pa kazi wataweza kuisimamia utekelezaji wake ipasavyo.
