Back to top

KENYA YAANZA KUHAMISHA RAIA WAKE ISRAEL

19 October 2023
Share

Kenya imeanzisha utaratibu wa kuwahamisha raia wake kutoka Israel, kufuatia kuzuka kwa mapigano, ambapo zaidi ya raia 500 wamesajiliwa na ubalozi wa Kenya nchini Israel, huku idadi kubwa wakiishi katika maeneo ambayo yamesalia salama na ambayo hayajaathiriwa na uhasama unaoendelea.

Kwa mujibu wa Afisa Mkuu anayehusika na masuala ya Mataifa ya kigeni katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya Roseline Njogu,Kundi la kwanza la Wakenya 11 limewasili.

Wakenya nchini Israel kimsingi wanajumuisha wanafunzi, watu binafsi katika hija za kidini, au wale wanaofanya programu fupi za utafiti wa kisayansi.