Back to top

KIBONA JELA MIAKA 30 KWA KOSA LA KULIMA BANGI, MBOZI

19 October 2023
Share

Mahakama ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imemtia hatiani na kumuhukumu kifungo cha miaka 30 Gerezani mshitakiwa Willison Kibona (36) kwa kulima Bangi.

Kibona alikamatwa 26 Disemba, 2022 nyumbani kwake Ihanda akiwa na miche ya Bangi 335 yenye uzito wa kilo 13.8 ambayo aliipanda kwenye nyumba yake. 

Mshtakiwa amehukumiwa kifungo hicho ili kukomesha ulimaji huo wa bangi.