Back to top

ICC YAFUTA MASHTAKA 20 YAKIWEMO YA MAUAJI

20 October 2023
Share


Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), imefutilia mbali mashtaka 20 yakiwemo ya mauaji, unyanyasaji na mateso dhidi ya Waziri wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Maxime Gawaka baada ya kukosekana kwa ushahidi na mashahidi waliopo.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama hiyo, Karim Khan, amesema kwamba anaondoa mashtaka yote dhidi ya Maxime Gawaka, kwa sababu hakuna tena sababu yoyote ya kuridhisha kuhukumiwa kwake kutokana na mashauri hayo.

Wakati wa kusikiliza shauri hilo mnamo mwezi Agosti, upande wa utetezi uliwaambia majaji kwamba waendesha mashtaka walikuwa wametoa ushahidi ambao unaweza kumuondolea hatia Mokom hata kabla ya kukamatwa kwake katika taifa jirani la Chad mwaka 2022.