Back to top

WATU WAWILI WAHUKUMIWA KUNYONGWA MOSHI.

23 October 2023
Share

Wakazi wawili wa vijiji vya Mbomai Wilaya ya Rombo Luka Kavishe na John Mremi wa kijiji.cha Kilema wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wamehukumuwa kunyongwa hadi kufa na Mahakama Kuu Kanda ya Moshi , katika kesi mbili tofauti za mauaji.

Hukumu hiyo imetolewa na Naibu Msajili wa Mahakama hiyo Bw. Omari kingwele, baada ya kuridhika na maelezo ya upande wa mashtaka, ulioongozwa na wakili wa serikali Frank Wambura na mashahidi wa pande zote katika kesi hizo.

Awali ilidaiwa kuwa Julai 30 mwaka 2017 jioni  Luka Kavishe alisababisha kifo cha marehemu Sepronia Kalisti wa kijiji cha Mbomai kwa kumbaka na kumlawiti kisha kumwingizia zaidi ya mara moja,  kitu butu sehemu zote za siri na kumjeruhi vibaya.

Katika hukumu yake Mh Kingwele amesema ameridhika na ushahidi wa mjukuu na mtoto wa marehemu Tatusa Emil, Tedy Tesha na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Huruma wilayani Rombo Dk. Wilbroad Kyejo.

Katika kesi nyingine mahakama hiyo imeridhika na ushahidi uliotolewa dhidi ya John Mremi, kwamba alishiriki katika mauaji ya mdogo wake, kwa kuwakaribisha nyumbani kwake siku ya tukio watu wasiojulikana, ambao walimpiga marehemu na kusababisha kifo chake.

Baada ya hukumu hiyo Bw. Kingwele, amesema washtakiwa wote wawili wana haki ya kukata rufaa mahakama ya juu kama hawakuridhika.