
Mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa shughuli za bima nchini TIRA imetangaza kuzifutia leseni ya biashara kampuni 4 udalali wa bima nchini kutokana na kampuni hizo kukiuka taratibu za uendeshaji wa biashara ya bima.
Kamishna wa bima wa mamlaka hiyo Baghayo Abdallah Saqware amesema makampuni hayo ya udalali yameshindwa kuwasilisha tozo za bima kwa makampuni ya bima.
Aidha Dakta Saqware amesema mamlaka hiyo inaendelea kushirikiana na Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai ili kuwapata na kuwachukulia hatua wamiliki wa kampuni nyingine mbili ambazo zimekuwa zikikwepa ukaguzi wa mamlaka hiyo.
Kampuni za udalali zilizofutiwa leseni ni Kampuni ya Hans, Kampuni ya Endeavour Kampuni ya Legend of East Afrika na kampuni Swift.