
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kushirikiana na madaktari Bingwa na Bobezi, kutoka nchini India kwa mara ya kwanza wamefanya upasuaji wa kupunguza uzito kwa wagonjwa wenye uzito uliokithiri.
.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Prof.Mohamed Janabi, ambapo amebainisha kuwa kilichofanyika ni ukubwa wa tumbo kupunguzwa kwa kutumia njia ya matundu na kwamba mgonjwa mmoja kati ya waliofanyiwa upasuaji huo aliruhusiwa kurudi nyumbani siku ileile.
.
Kuhusu gharama za upasuaji huo, Prof.Janabi amesema kwa hapa Tanzania unafanyika kwa gharama ya chini ya Tsh. Mil.15, ikilinganishwa na nchi zingine ambazo hufanya upasuaji huo kwa gharama ya kati ya Tsh. Mil. 50 hadi Mil. 70.
