
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei mpya za Mafuta zilizoanza kutumika leo Novemba 01, 2023, ambapo kwa Mkoa wa Dar es Salaam, mafuta ya Petroli ni Tsh. 3,274/= yakiwa yameshuka kutoka Tshs. 3,281/= mwezi uliopita, huku mafuta ya Dizeli yakiwa ni Tsh. 3,374/= yakiwa yameshuka kutoka Tsh. 3,448/= mwezi uliopita.
.
EWURA imesema kushuka kwa bei hiyo ni kutokana na kupungua kwa bei ya mafuta katika soko la dunia kwa wastani wa 5.68% na gharama za uagizaji kwa wastani wa 13% kwa petroli, 25% kwa dizeli na uamuzi wa wazalishaji wakubwa wa mafuta duniani (OPEC+) kupunguza uzalishaji na vikwazo vya kiuchumi ambavyo nchi ya Urusi imewekewa.