
Salma Abdallah (37), Mkazi wa Lumala wilayani Ilemela, mkoani Mwanza, amefikishwa katika Mahakama ya wilaya hiyo na kusomewa shtaka la kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi.
.
Akimsomea shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo, Amani Sumari, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Monika Mweli, amesema mshtakiwa alitenda kosa hilo kati ya Oktoba 01, 2023 na Oktoba 27, 2023, katika eneo la Lumala, wilayani Ilemela.
.
Baada ya kusomewa shtaka hilo, mshatakiwa amekana na kurejeshwa rumande kutokana na kutokidhi masharti ya dhamana ambapo alitakiwa kuwa na wadhamini wawili na kila mmoja kusaini bondi ya maneno ya shilingi milioni mbili kwa kila mmoja, kitambulisho pamoja na barua ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa ambapo mshtakiwa alijibu kuwa hana wadhamini hao.
.
Hakimu, Sumari ameahirisha shauri hilo hadi Novemba 13, 2023, ambapo mshtakiwa atasomewa maelezo ya awali ya shtaka linalomkabili.
