Back to top

WAFUGAJI WAFUGE KIMKAKATI KULINDA MAZINGIRA

01 November 2023
Share

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.Selemani Jafo awapa rai wafugaji kufuga kimkakati ili kulinda mazingira kwa kuwa ufugaji endelevu usioathiri hifadhi ya mazingira utasaidia katika kuepusha migogoro baina ya wakulima na wafugaji nchini.

Waziri Jafo hayo Jijini Dodoma ambapo amesema kuwa wafugaji nchini hawana budi kuwa mabalozi wazuri na kuungano mkono juhudi za Serikali za kuhifadhi mazingira kwa kufanya shughuli za ufugaji wenye tija kwa maendeleo endelevu.

Amewataka wafugaji nchini kuunga mkono juhudi za Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye anaendelea kuiletea nchi maendeleo ikiwemo kuendeleza sekta ya maji.

Kwa upande mwingine Dkt.Jafo amewahimiza wafugaji ambao wamepata ufadhili kutumia fursa ya Mkutano wa 28 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 28) kushiriki kikamilifu.

Amesema kuwa mkutano huo unaotarajiwa kufanyika Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Novemba 28 hadi Desemba 5, 2023 utakuwa ni adhimu ya kuitangaza nchi yetu namna Tanzania inavyofanya ufugaji rafiki wa mazingira.

Hali kadhalika Waziri Jafo ametoa wito kwa CHAMAUTA kulitumia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kupata uelewa kuhusu kanuni na zinazosimamia mazingira ili kuepuka shughuli zinazoharibu mazingira.

Amesema kupitia miradi mbalimbali Serikali imekuwa ikichimba malambo kwa ajili ya kunyweshea mifugo hususan katika maeneo yenye ukame hatua inayosaidia kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe.Remidius Mwema aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ameipongeza Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kusimamia utekelezaji wa uhifadhi wa vyanzo vya maji.

Amesema kuwa mikakati ya kuhifadhi vyanzo vya maji katika eneo la Makutupora inaendelea na kuwa tayari chanzo hicho kimeanza kutoa asilimia 61 ya mahitaji ya maji kwa mkoa. 

Aidha, Mhe.Mwema amesema kuwa Serikali ya Mkoa inaendelea na Kampeni ya Kukijanisha Dodoma ambapo inaendelea kuandaa vitalu vya miche ili kukabiliana na upungufu wa miche.

Naye Mwenyekiti wa CHAMAUTA amesema chama hicho kimemtunuku Waziri Jafo kadi ya uanachama wake na mlezi kumuomba kuwa mlezi wake kutokanamchango wake na Ofisi kwa ujumla.