
Kichwa kipya cha kwanza cha treni ya umeme chenye namba ya usajili E6800-01 kilichoundwa na kampuni ya ‘Hyundai Rotem Company’ (HRC) ya nchini Korea Kusini, kimewasili nchini.
.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Shirika la Reli Tanzania (TRC), limebainisha kuwa liliagiza vichwa vipya 17 vya umeme, vyenye namba ya usajili E6800-01 hadi E6800-17 kwa ajili ya Reli ya Kiwango cha Kimataifa (SGR), ambapo mfumo wa uendeshaji unaotumika katika kichwa hicho ni nishati ya umeme, wenye msongo wa kilovoti 25 na kitakuwa na nguvu ya kilowati 5,000 sawa na nguvu ya 6,800 kwa kipimo cha ‘Horse Power’.
.
Aidha, Shirika hilo limesema linatarajia kufanya majaribio ya kichwa hicho, kati ya Dar es Salaam na Morogoro na baadaye Dar es Salaam hadi Dodoma, baada ya kukamilisha ukaguzi wa kichwa na mafunzo ya uendeshaji kwa Madereva mapema mwezi Disemba 2023.

