
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, imewakamata watu wanaojihusisha na utengenezaji wa biskuti kwa kuchanganya na bangi katika eneo la Kawe, mkoani Dar es Salaam, ambapo imebainisha kuwa watuhumiwa hao walikutwa wakiendelea na uzalishaji wa biskuti hizo kwa kutumia mtambo mdogo wa kusaga skanka (Neno la mtaani linalotambulisha aina ya bangi yenye kiwango kikubwa cha sumu ikilinganishwa na bangi ya kawaida) na vifaa vya kutengenezea biskuti hizo.
.
Mamlaka hiyo imesema Dawa hiyo ya kulevya inatokana na kilimo cha bangi mseto, ambapo 75% ni bangi aina ya sativa na 25% ni aina ya indica, huku kiwango chake cha sumu kikitajwa kuwa ni 45% ikilinganishwa na bangi ya kawaida ambayo kiwango chake cha sumu ni kati ya 3% mpaka 10%.

