Back to top

MFUMUKO WA BEI WAPUNGUA KUTOKA 3.3% HADI 3.2%

08 November 2023
Share

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba 2023, umepungua hadi 3.2%  kutoka 3.3% kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba 2023.
.
NBS imesema kupungua kwa mfumuko huo, kumechangiwa na kupungua kwa mfumuko wa bei kwa baadhi ya bidhaa za chakula kwa kipindi cha mwaka ulioishia mwezi Oktoba 2023, ambapo baadhi ya bidhaa za vyakula zilizoonesha kupungua ni pamoja na mchele ambao umepungua kutoka 7.6% hadi 4.4%, Samaki wabichi kutoka 8.0% hadi 7.1% na Dagaa wakavu kutoka 13.5% hadi 11.0%.