Back to top

TMDA SASA KUSIMAMIA MADUKA YA DAWA

09 November 2023
Share

Serikali imeondoa usimamizi wa maduka ya Dawa kutoka Baraza la Famasi na kupeleka majukumu hayo kwenye Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), ikiwa ni mikakati madhubuti ya kukabiliana na usugu wa vimelea dhidi ya dawa mwilini (Antimicrobial Resistance AMR), tatizo ambalo limeonekena kuwa tishio kubwa la afya kwa jamii ya Watanzania.
.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya, Mhe.Ummy Mwalimu kupitia ukurasa wake wa X.Com (iliyokuwa Twitter), ambapo amebainisha kuwa kumekuwepo na matumizi yasiyo sahihi ya dawa nchini, hivyo kufanya dawa nyingi za Antibiotiki kuwa na ufanisi mdogo katika kutibu magonjwa. 
.
Waziri Ummy, amesema Pamoja na uelewa mdogo wa wananchi kuhusu matumizi sahihi ya dawa za Antibiotiki, tatizo hilo kwa kiasi kikubwa, limekuwa likichochewa na baadhi ya wataalam kwenda kinyume na kanuni na miongozo ya taaluma yao.
.
Aidha, Waziri Ummy amewataka wahudumu wa Afya hasa Madaktari na Wafamasia kusimamia jukumu hilo ili Watanzania wapate uelewa juu ya matumizi sahihi ya dawa.