
Rais wa Ureno Marcelo Rebelo de Sousa, amelivunja bunge la taifa hilo na kuitisha uchaguzi wa mapema, ikiwa ni siku mbili tu tangu Waziri Mkuu Antonio Costa kutangaza kujiuzulu na serikali yake iliyogubikwa na kashfa ya rushwa.
Rais huyo ametoa tangazo hilo alipohutubia taifa kupitia televisheni,ambapo amesema uchaguzi mpya huenda ukafanyika Machi 10, 2024
Waziri Mkuu aliyejiuzulu Antonio Costa aliiongoza Ureno tangu mwaka 2015, na kushinda kwa kishindo kwenye uchaguzi wa Julai mwaka uliopita.
Alijiuzulu mara moja kufuatia msako mkali wa polisi siku ya Jumanne, kama sehemu ya uchunguzi wa tuhuma za rushwa ambapo mkuu wake wa utumishi pamoja na watu wengine wanne walikamatwa, huku waziri mmoja akitajwa kama mtuhumiwa.
